Mwanamitindo wa kiitaliano mwenye asili ya nchi ya Serbia Claudia Romani ameamua kuachana na kazi ya uanamitindo na kuamua kujiunga na kazi ya uamuzi wa mpira wa miguu.
Mwanamitindo huyo alifanya mtihani wa majaribio na kufaulu kuwa mwamuzi wa mchezo wa soka na sasa huenda siku za hivi karibuni tukaanza kuyaona maujuzi yake katika fani yake hiyo mpya.
Claudia Romani, mwenye umri wa miaka 32, ni mmoja kati ya wasichana warembo sana nchini Italy lakini ameamua kuachana na kazi yake hiyo ya urembo na kuamua kuwa mwamuzi wa mchezo wa soka mapema mwaka huu na tayari amekwishafanya mtihani na kufaulu vizuri hivyo anachokisubiri sasa ni kupangiwa kazi kwaajili ya kuisimamia michezo mbalimbali.
Kutokana na kufaulu huko Romani sasa anavigezo vya kuwa mwamuzi katika michezo ya Serie A na Serie B, ambazo ndizo ligi za daraja la juu zaidi nchini Italy.
Alipoulizwa na waandishi wa habari juu ya majukumu yake mapya hayo anayotarajiwa kuyaanza siku za hivi karibuni kichuna huyo alikua na majibu mafupi sana yaliyowafanya waandishi watosheke na kuishiwa pozi ‘Kukimbia huku na kule kuuzunguka uwanja pamoja na wachezaji wote 22 waliomo uwanjani na kutoa maamuzi kwenye makosa mbalimbali yatakayokua yakitokea dimbani ni nafasi adhimu kwangu na kwa maisha yangu kwa ujumla,’
Historia inaonesha kuwa hakuna mwamuzi mwanamke aliyewahi kushika kipyenga kwenye ligi ya Serie A lakini pia haiko sheria inayomzuia mwanamke kuifanya kazi hiyo.
Post a Comment