David De Gea yuko njiani kutua ndani ya klabu ya Real Madrid mwishoni mwa msimu huu wakati klabu yake ya sasa ya Manchester United ikijiandaa kumsainisha Victor Valdes kama mbadala wake ndani ya klabu hiyo.
Madrid imeendelea kukomaa na msimamo wake wa kutaka kumjumuisha kikosini De Gea kufuatia kiwango bora kilichooneshwa na mlinda mlango huyo siku za hivi karibuni akiwa na kikosi cha United.
Taarifa zilizozagaa kwenye vyombo vya habari siku za hivi karibuni ni juu ya uwezekano wa golikipa huyo kurejea nchini Hispania lakini safari hii akirejea Santiago Bernabeu huku mkataba wake wa sasa na mashetani wekundu hao ukiwa unamruhusu mchezaji huyo kufanya mazungumzo na klabu yoyote ile kwakuwa unaelekea ukingoni.
United inajiandaa kumsajili golikipa wa zamani wa klabu ya Barcelona Victor Valdes ambaye siku za hivi karibuni amekuwa akifanya mazoezi na mashetani wekundu hao na huenda dili lake likakamilika siku chache zijazo.
Post a Comment