Matumaini ya mshambuliaji raia wa Colombia Radamel Falcao kusaini mkataba wa muda mrefu na klabu ya Manchester United yameanza kufutika kutokana na kali ya kiafya ya mshambuliaji huyo mwenye sanaa ya ufungaji kuwa sio nzuru kwa ujumla wake.
Taarifa kutoka ndani ya moja ya vyanzo vya kuaminika ndani ya klabu ya Manchester United zinadai kuwa hali ya kifundo cha mguu cha mchezaji huyo si nzuri sana kwani inamlazimu kufunga barafu kwenye jeraha lake hilo kila anapomaliza mechi au mazoezi na klabu hiyo.
Klabu ya Manchester United ilmsainisha kwa mkopo wa muda mrefu kotoka klabu ya AS Monaco ya nchini ufarasa ikiwa nia mara tu baada ya kutoka kuuguza jeraha la kifundo cha mguu lililomsababishia kukosa mashindano ya kombe la Dunia nhini Brazil.
Wakati klabu ya Man U sasa ikiwa katika dimbwi la fikra aidha kumsajili au kutokumsajili kwa mkataba wa muda mrefu mchezaji huyo, lakini taarifa zinadai kuwa Falcao anaonekana kukalia kuti kavu ndani ya klabu hiyo kutokana na mwendelezo wa majeraha hayo yanayomsibu mshambuliaji huyo.
mpaka sasa mshambuliaji huyo raia wa Colombia amecheza michezo mitano tu miwili kati ya hiyo akitokea benchini tangu klabu yake hiyo ilipomnunua kwa mapesa mengi kutoka Ufaransa huku akiifungia timu hiyo goli moja tu kwenye mchezo amabao Man Utd ilicheza na Everton.
Post a Comment