Mwezi Januari unatajwa kuwa ni mmoja kati ya miezi mabayo mameneja na wamiliki wengi wa vilabu wanapenda kufanya usajili wao kwani inaaminika kuwa katika mwezi huo hata bei ya wachezaji inakua nafuu kidogo.
Mpaka sasa mimi binafsi sijaelewa mantiki ya wachezaji kushuka thamni katika kipindi hicho lakini hii ni hali ya kawaida ambayo imekua ikijitokeza miaka kadha sasa na tumeshuhudia wachezaji wengi wakiuzwa kwa bei ya chini au ya kawaida kabisa tofauti na bei inavvyokua katika vipindi vingine vya usajili.
Kwa mujibu wa taratibu za kiusajili zilivyo barani Ulaya zinasema kuwa iwapo mchezaji atakua ametimiza umri wa miaka 23 na mkataba wake utakua umebakiza miezi 6 au chini ya hapo anaweza kusaini mkataba wa awali na klabu inayoonesha nia ya kutaka kumsajili na mwisho wa mkataba wake huo atakua huru kuhamia klabu hiyo aliyosainiana nayo mkataba huo wa awali akiwa kama mchezaji huru.
Ifuatayo ni orodha ya wachezaji ambao utakapofika mwezi wa January watakua wako huru kusaini mikataba hiyo ya awali na vilabu vitakavyoonesha nia ya kuzitaka huduma zao.
1. Sami Khedira (Real Madrid)
2. Fabian Schar (Fc Basel)
3. Giorgio Chiellini (Juventus)
4. Dani Alves (Fc Barcelona)
5. Fabian Delph (Aston Villa)
6. Ron Vlaar (Aston Villa)
7. Klaas-Jan Huntelaar (Fc Schalke 04)
8. Luiz Adriano (Shakthar Donetsk)
9. John Terry na Steven Gerrard (Chelsea na Liverpool)
Wachezaji wengine wanaomaliza mikataba yao na wanawea kupatikana mnamo mwezi January ni Nigel de Jong,
Yehven Konoplyanka, Andre-Pierre Gignac, Michael Carrick, Glen Johnson,
Emmanuel Adebayor, Mikel Arteta, Winston Reid, Andre Ayew, Ignazio
Abate, Sergio Romero, Yoann Gourcuff, Eduardo Vargas, Stephan
Lichtsteiner na Maxi Pereira.
Post a Comment