Wamiliki wa klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza wameanza kufikilia uwezekano wa mumtimua meneja wa timu hiyo Brendan Rodgers kufuatia mwenendo usio eleweka wa klabu hiyo tangu mwanzoni mwa msimu huu.
Tuvuti moja ya nchini Italia Tuttomercato imeandika kuwa wamiliki wa klabu hiyo hawalidhishwi na mwenendo wa meneja huyo wa zamani wa klabu ya Swansea.
Rodgers kwa sasa amekua hana sapoti kutoka kwa uongozi wa klabu hiyo lakini pia mashabiki wa timu hiyo kutokana na matokeo mabovu kwani mpaka sasa klabu hiyo imeshinda takribani michezo minne tu katika michezo 11 ya ligi kuu ya nchini Uingereza iliyokwisha cheza, lakini pia ikiwa na mwenendo wa kusuasua.
Taarifa zinasema kuwa mpaka sasa hakuna maamuzi yoyote yaliyofikiwa juu ya mustakabali wa mwalimu huyo licha ya kuwa bado yuko katika wakati mgumu sana ndani ya timu hiyo. Lakini inasemekana kuwa lolote linaweza kutokea kwenye mustakabli wa meneja huyo.
Post a Comment