0


Messi celebrates scoring his first goal against Ajax on Wednesday night in the 2-0 win in AmsterdamNa Oswald Ngonyani.

Kwa siku za karibuni kumekuwa na hali ya ukinzani mkubwa wa kimtazamo miongoni mwa mashabiki wengi wa mchezo wa soka hususan wanazi wakubwa wa wachezaji fulani wawili kutoka katika klabu mbili tofauti zinazocheza ligi moja barani Ulaya.

Wanazi hao wamekuwa hawaridhiki pale mchezaji mmoja anapozungumzwa kwa mazuri. Mioyo yao huingiwa na gubu na hata kujikuta wakionesha chuki ya wazi kwa mchezaji anayesifiwa, lengo hasa ni kutaka kuzipambanua sifa fulani za mchezaji wanayemkubali.

 
Hivi ndivyo mchezo wa soka ulivyo, mchezo ambao mbali na kuwa na mashabiki wengi ulimwenguni kote lakini bado umetawaliwa na vibweka lukuki, vibweka ambavyo kila kunapokucha vinazidi kushika kasi.

Mpaka leo hii bado kuna mvutano mkali kuhusu umaridadi wa wachezaji hawa ‘Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Lionel Messi wa Barcelona’.

 Dynamic duo: Messi and Neymar chat during training
Kiuwezo wa ndani ya uwanja kila mmoja ana upekee wake unaompambanua na hata kuonekana kuwa bora zaidi ya mwingine. Nakumbuka wakati fulani niliwahi kuandika makala ya uchambuzi kuhusu wanandinga hawa.

Ni katika makala yale ndipo nikagundua kitu fulani kuhusu wachezaji hawa. Si watu wa mataifa mengine pekee, hata watanzania wengi wamegawanywa katika pande mbili za uhusuda wao kwa hawa jamaa.

 
Maoni ya watu kutoka pande zote za nchi kuhusiana na unazi wao kwa wachezaji hawa ni vitu vilivyonifanya nielewe kuwa kweli akina Messi na Ronaldo ni wachezaji bora wa dunia kwa sasa.

Utamu wa mchezo wa soka kama unavyonakshiwa na uwepo wa historia na rekodi nyingi zenye kutia hamasa huzidi zaidi pale rekodi fulani zinapovunjwa na hata kuzua gumzo kwa wanaozifuatilia rekodi hizo. Hivi ndivyo mchezo wa soka ulivyo, karibu kila siku mambo mapya yanaibuka na hata kujenga historia kamambe yenye kutia hamasa.

 Signing on: Messi signs autographs for fans at the open training session
Achana na sifa tukufu wanazopewa akina Pele na Maradona, nadhani hao jamaa wana upekee wao unaowafanya wawe maarufu mpaka leo hii kutokana na kile ambacho waliwahi kukifanya enzi za ujana wao.

Nyuma ya watu hawa kuna mtu fulani wa umri wa makamo ambaye hazungumzwi sana, anaitwa Raul Gonzalez kipenzi cha mashabiki wengi wa soka nchini Hispania ambaye alipewa sifa iliyotukuka sana pale Santiago Bernabeu na hata kujikuta akiwa mchezaji wa miaka mingi zaidi wa Klabu ya Real Madrid.

 
Mpaka tunaanza siku ya kwanza ya wiki hii, Mwanamume huyu alikuwa anashikilia rekodi fulani, rekodi ambayo alidumu nayo kwa muda mrefu sana kutokana na wachezaji wengi wa sasa kuonekana kutokuwa na ‘mzuka’ wa kuivunja rekodi hiyo.

Mashabiki wengi wa Real Madrid walikuwa na hamu kubwa ya kumuona mchezaji wao kipenzi akiivunja rekodi hiyo. Nadhani kuna hali fulani ya chuki ilikuwa imewatawala ndani ya mioyo yao, hawakuwa tayari rekodi ya kipenzi chao Gonzalez ivunjwe na mtu wanayemchukia sana, Lionel Messi.

 Head down: Messi gets his head over the ball and shoots during training
Mashabiki wengi wa Madrid wanamchukia Messi kwa sababu ya maneno yanayozungumzwa mara kwa mara na baadhi ya watu wa familia ya mchezo wa soka kuwa Messi ni zaidi ya Ronaldo. Kwao kauli hizo ni kama dhihaka, hawazitaki kuzisikia hata kidogo. 



Wanaamini Ronaldo wao ndiye fundi pekee wa mpira kwa sasa kuliko wengine wote, hii ndiyo imani yao na kamwe hawawezi kubadilika. Hawakutaka Messi atangulie kuvunja rekodi ile, walitaka kipenzi chao Ronaldo afanye vile lakini haikuwezekana.

 
Raul alikuwa akishikilia rekodi ya kufunga mabao 71 na kuwa mfungaji mwenye mabao mengi zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya tangu kuanzishwa kwake miaka 60 iliyopita.



Kabla yake Messi alikuwa hapewi nafasi, lakini mabao mawili aliyofunga Messi wakati Barcelona ikiitwanga Ajax kwa mabao 2-0 kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, yamesitisha ndoto za Ronaldo aliyekuwa kipewa nafasi kubwa.



 Ronaldo celebrates scoring his 17th league goal of the season against Granada on Saturday

Muargentina huyu aliyekuzwa pale Lamasia amefikisha mabao 71 huku Ronaldo akibaki na mabao 70 na anachotakiwa sasa ni kufunga zaidi ili kumfikia Messi na Raul na ikiwezekana kuwapita wote vinginevyo ataendelea kusubiri kwa muda.

Takwimu za sasa za ufumaniaji wa magoli mengi katika UEFA zinamweka Messi wa Barcelona katika nafasi ya kwanza akiwa amelingana na Gonzalez kwa kuwa na magoli 71 huku Ronaldo akiwa na magoli 70.

 Lionel Messi runs away in celebration after scoring Barcelona's second goal against Ajax on Wednesday
Nyuma ya wachezaji hawa watatu kuna wengine wawili ambao wanafuatia. Nyota wa zamani wa Manchester Uniter Ruud Van Nistelrooy mwenye magoli 56 na Thiery Henry, mfaransa aliyewahi kuvuma pale Emirates akiwa na hazina ya magoli 50 kwa sasa.

Kimsingi, rekodi ya Raul Gonzalez ambayo kwa miaka mingi sasa imekuwa ikisakwa kwa udi na uvumba imekwishavunjwa tayari. Ninaamini tunakwenda kushuhudia rekodi mpya kabisa ambayo mmoja kati ya wachezaji hawa wanaochuana kwa sasa ataiweka na hata kulifanya jina lake kutamkwa mara kwa mara katika vinywa vya mashabiki wengi wa mchezo wa soka duniani kote.

 
Ni wazi kuwa, wote wawili wanaweza wakaweka historia ya pekee zaidi katika ufumaniaji wa nyavu katika michuano ya UEFA lakini pia wachezaji wengine wana nafasi pia ya kuifikia rekodi hii na hata kuanza ukurasa mpya wa rekodi mpya zenye kuongeza chachu katika mawanda ya soka la sasa.

Naomba kutamatika.


Post a Comment

 
Top