0
Tom Cleverley

DAVID MOYES rasmi ameteuliwa kuifundisha klabu ya Real Sociedad inayokipiga kwenye ligi kuu nchini Hispania, Kama ilivyo ada kwa mameneja wengi kupenda kufanya kazi na wachezaji anaowafahamu pia David Moyes ameshindwa kuzizuia hisia zake za kutaka kufanya kazi na wachezaji kadhaa lakini wote akiwa tayari amekwishafanya nao kazi kwenye klabu ya Manchester United.

Mara tu baada ya kuthibitishwa kuchukua mikoba ya kikinoa kikosi cha mashetani wekundu wa Manchester United Msicotland huyu alihama na benchi lake lote la ufundi na kuanza mchakato wa kutaka kuwajumuisha kikosini wachezaji wamwili kutoka klabu yake ya zamani ya Everton ambao ni mlinzi Leighton Baines na kiungo Marouane Fellaini.

Moyes alifanikiwa kuinasa saini ya Mbeligiji Marouane Fellaini kwa kulazimishwa kulipia ada ya uhamisho inayokadiliwa kufikia kiasi cha paundi milioni 27 ili kukamilisha dili hilo.Kwa sasa mambo ni tofauti kidogo kwani Moyes yuko kwenye klabu ambayo haina mapesa mengi kama ilivyokuwa Manchester United hivyo ili kuhakikisha kuwa mambo yanakwenda sawa basi lazima Moyes awaangalie wachezaji chipukizi watakaoweza kupatikana kwa ghalama nafuu.

Kutokana na hali hiyo inayomkabili sasa ndani ya majukumu yake mapya ndani ya klabu hiyo wafuatao ni wachezaji watatu kutoka klabu ya Manchester United ambao meneja David Moyes amewataja Tom Cleverley,Adnan Januzaj na Ashley Young, kuwa ni miongoni mwa wachezaji anaowataka kufanya nao kazi ndani ya klabu yake hiyo mpya.

Post a Comment

 
Top