0

as_moyes2
Klabu ya Real Sociedad hii leo inatarajiwa kumtangaza rasmi kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United na Everton David Moyes kuwa meneja mpya wa klabu hiyo hii leo.

Taarifa zimesema kuwa tayari Meneja huyo amekwishafanya makubaliano yote ya kimsingi na mabosi wa klabu ya Real wiki iliyopita alipokwenda Nchini Spain kwaajili ya mazungumzo hayo yaliyokwenda sawasawa.

Kocha huyo wa zamani wa klabu ya Everton aliyetimuliwa na mabosi wa klabu ya Manchester Unitem mnamo mwezi April mwaka huu ikiwa ni nusu tu ya msimu ndani ya Old Trafford tayari alishazungushwa kwenye maeneo yote muhimu ya klabu hiyo kwaajili ya kupafahamu zaidi kabla ya kurejea kwao na hii leo anatarajiwa kutangazwa rami.

Post a Comment

 
Top