0
as_messi2
Alex Song amewaacha vinywa wazi waandishi wa habari pale alipowaambia waandishi hao kuwa yuko kwenye mchakato wa kuwashawisi mabosi zake wa klabu yake anayoitumikia kwa mkopo ya West Ham United wamsajili mchezaji bora wa Dunia wa miaka kadhaa iliyopita Muajentina Lionel Messi.

Song anatarajiwa kurejea ndani ya klabu ya Barcelona majira yajayo ya joto lakini ameendelea kusisitiza kuwa anajisikia furaha sana ndani ya West Ham kuliko vile hali ilivyo kwenye klabu yake ya Barcelona.

West Ham United iliyo chini ya meneja Sam Allardyce panaonekana kuwa ni sehemu inayompa raha sana Song na hivyo kusahau shida zote alizokuwa akikumbana nazo ndani ya Wakatalunya haona hivyo kujikuta akitaka kumshawishi Lionel Messi aweze kutua ndani ya timu hiyo ili nae aje aishi maisha ya furaha kama ilivyo aishivyo yeye kutokana na mazingira yanayomkabili Messi ndani ya Barcelona kwa sasa.

Post a Comment

 
Top