Falcao aliyesajiliwa kwa mkopo wa paundi milioni 6 kutoka klabu ya AS Monaco kwa sasa anapambana kurejea katika hali yake ya kawaida kutoka kwenye maumivu ambayo yalimfanya kuyakosa mashindano ya kombe la Dunia kule nchini Brazili mwaka huu.
Pekerman,ambaye kikosi chake kinakwenda kuvaana na Marekani kwenye mchezo wa kirafiki usiku huu kwenye dimba la Craven Cottage nchini Uingereza atakua bila ya mshambuliaji wake wakutumainiwa wa timu hiyo Radamel Falcao, aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo:
"Falcao yukokatika moja kati ya vilabu bora kabisa Duniani inayoshiriki kwenye ligi ambayo ni moja kati ya ligi bora Ulimwenguni lakini pia yuko pamoja na mmoja kati ya mameneja bora kabisa ulimwenguni Louis van Gaal ambaye ukitaka kujua ubora wake jaribu kutazama matokeo ya timu ya taifa ya Uholanzi kwa sasa."
"Kucheza Uingereza ni kitu kipya kwake kinachohitaji mazoea kidogo lakini ni mtu ninayemtarajia kupata uzoefu huo siku chache zijazo na hatimaye kuanza kujipatia mafanikio."
"Ninachoweza kuwaambia kuwa wanachotakiwa kukifanya klabu ya Manchester United ni kumvumilia Falcao kuepukana na maswahibu yanayomsibu kwa sasa, arejee kwenye kiwango chake na wao waanze kunufaika na matunda yatakayotokana na uwezo wa mchezaji huyo."
Post a Comment