0
The Manchester United striker had taken part in training, but is not fully fit according to his managerMlinzi wa kati wa klabu ya PSV Jeffrey Bruma anatarajiwa kuchukua nafasi ya mlinzi Bruno Martins Indi kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi kwaajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Mexico na Latvia, Wakati kocha wa timu hiyo ya taifa ya Uholanzi pia Guus Hiddink amewatema kikosini mwake wachezaji Robin van Persie na Jordy Clasie kwaajili ya mchezo huo wa kirafiki wa hapo kesho dhidi ya Mexico unaotarajiwa kufanyika kwenye dimba la Amsterdam Arena. 

Watakapo maliza mchezo dhidi ya Mexico kwenye dimba la Amsterdam Arena kikosi hicho cha Hiddink watakua wakikipiga dhidi ya timu ya taifa ya Latvia mchezo unaotarajiwa kuchezwa kwenye dimba hilohilo la Amsterdam Arena siku ya Jumamosi ukiwa ni mchezo kwaajili ya kufuzu kwa michuano ya Ulaya mnamo mwaka 2016.

Wakati mlinzi wa klabu ya FC Porto ya nchini Ureno Martins Indi ambaye alikua muhimili imara kwenye sehemu ya ulinzi ya timu ya taifa ya Uholanzi kwenye michuano ya kombea la Dunia akiachwa kujumuishwa kikosini kutokana na kuwa mgonjwa nafasi yake sasa inatarajiwa kuzibwa na Bruma.

Robin van Persie leaves the Dutch training session with fitness coach Rene Wormhoudt on Tuesday
Bruma hajapatiwa nafasi ya kuwemo kwenye kikosi cha The Oranges tangu October 2013 na mara kadhaa alitumika kama mchezaji wa akiba ambaye hakuwahi kupata nafasi wakati wa kampeni za kufuzu kwaajili ya michuano ya kombe la Dunia.

Taarifa zinadai kuwa Van Persie na Clasie wameachwa kwenye kikosi kitakachocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mexico kutokana na kuwa na maumivu madogo ya misuli ya paja hivyo kuwapa nafasi ya kupumzika ili waingie kwenye mchezo muhimu wakiwa fiti.

Van Persie, who played 90 minutes on Saturday, says he wants to play professionally until he is 40
"Wachezaji hawa wawili wote wana matatizo yanayo fanana,Van Persie amefanya mazoezi hii leo japo hajafanya mazoezi kwa muda wote tuliojipangia ili kumpa nafasi ya kupumzika na kurejea katika hali yake ya kawaida." alisema kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi Guus Hiddink alipokuwa akiongea na waandishi wa habari.

Post a Comment

 
Top