0
Ander Herrera (2nd left), in action in the reserves on Tuesday as he continues his recovery from injury
Kiungo wa klabu ya Manchester United Ander Herrera atatakiwa kusafiri kwenda nchini Hispania kuhudhuria mahakamani kwaajili ya kutoa ushahidi wa kesi ya upangaji wa matokeo.

Herrera mmoja kati ya wachezaji 28 wanaotakiwa kuhudhuria mahakamani katika jiji la Valencia mapema mwakani ili kutoa ushahidi wao kuhusiana na kashfa iliyopo sasa ya upangaji wa matokeo kwenye mchezo amabao yeye aliucheza mnamo mwezi May 2011.

Meneja wake wa zamani Javier Aguirre, ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha timu ya taifa ya Japani, na nahodha wa sasa wa klabu ya  Atletico Madrid, Gabi ni miongoni mwa watu watakao takiwa kuhudhuria mahakamani hapo kwaajili ya kutoa ushahidi wa kesi hiyo.

 Herrera, in action for Zaragoza against Barcelona star Lionel Messi, is set to appear in court next year
Zaragoza walitakiwa kushinda mchezo wao wa mwisho wa ligi ya msimu wa mwaka 2010-2011 ili kumaliza katika nafasi za juu za msimamo wa ligi kitu ambacho walikifanikisha pale ambapo walifanikiwa kuifunga klabu ya Levante jumla ya magoli 2-1 ugenini kwenye mchezo ambao Herrera alicheza kwa takribani dakika 72 kabla ya kufanyiwa mababdiliko.

Kabla ya mchezo huo kulikua na taarifa zilizotolewa na Raisi wa klabu ya Deportivo, Augusto Lendoiro ambaye ilishuhudiwa timu yake ya Deportivo ikipoteza nafasi mara baada ya ushindi huo wa Zaragoza kuwa Raisi mwenzake wa klabu ya Real Zaragoza, Agapito Iglesias alikua ametembeza mlungula ili timu yake ipate matokeo kwenye mchezo huo

Former Zaragoza president Agapito Iglesias (right) remains at the centre of an anticorruption investigation

Mwezi uliopita nahodha wa zamani wa klabu ya Real Zaragoza Gabi alikiri kupokea kiasi cha pesa kwenye akaunti yake ya Benki kutoka kwa Iglesias ikiwa ni wiki moja kabla ya mchezo huo kufanyika.

Ander Herrera anatajwa kuwa ni mmoja kati ya wachezaji saba ambao walipokea mlungula huo pamoja na meneja wao wa wakati huo Aguirre.

 Former Zaragoza captain Gabi, now at Atletico Madrid, admitted he received a sum of money from Iglesias



Post a Comment

 
Top