0
Angel di Maria (left) took part in Manchester United training on Friday after recovering from a foot injury
Louis van Gaal amethibitisha kuwa kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo Muajentina Angel Di Maria huenda asiwemo kwenye kikosi cha klabu ya Manchester United kitakachovaana na klabu ya Stoke siku ya Jumanne Usiku.

Di Maria, alitolewa mnamo dakika ya 14 tu ya mchezo baina ya klabu ya Manchester United na  Hull City ikishuhudiwa mashetani wekundu hao wakipata ushindi wa jumla ya magoli 3:0 mara baada ya kupata maumivu ya misuli ya paja alipokua akijaribu kuipangua ngome ya klabu ya Hull.

 "Angel huenda akawa njea kwenye mchezo wetu dhidi ya Stoke,  Van Gaal aliiambia tuvuti ya klabu ya Manchester United huku akithibitisha kuwa nahodha wa klabu hiyo Muingereza Wayne Rooney anatarajiwa kuwa fiti kwenye mchezo huo kutokana na ripoti ya awali ya matabibu ikidai kuwa mshambuliaji huyo alipata majeraha madogo ambayo hayatamfanya kuukosa mchezo huo."


Post a Comment

 
Top