Meneja wa klabu ya Arsenal Mfaransa Arsene Wenger anethibitisha kurejea dimbani kwa mshambuliaji wake raia wa Ufaransa Olivier Giroud kutoka kwenye majeraha yake yaliyokuwa yakimsibu siku ambayo washika mitutu hao watakapokua wakipambana na mashetani wekundu wa Manchester
United wiki mbili zijazo.
Taarifa za awali za kitabibu zilikua zikidai kuwa mshambuliaji huyo atakua nje ya uwanja mpaka mwezi wa January kutokana na maumivu yake ya mguu yaliyokuwa yakimkabili.
Giroud anaonekana kurejea kwenye hali yake ya kawaida mapema sana kuliko ilivyodhaniwa awali na meneja wa timu hiyo Arsene Wenger amethibitisha kurejea kwa mshambuliaji huyo na amesema kuwa rasmi ataanza mazoezi wiki ijayo.
Arsenal inatarajiwa kusafiri kwenda kuwavaa vijana machachari wa Swansea mwishoni mwa wiki kabla ya wachezaji kujiunga na timu zao za taifa kwa medani za kimataifa na hivyo kumpa nafasi mshambuliaji huyo kuwa na wiki tatu za kujiweka sawa kabla ya kurejea dimbani kwenye siku ambayo washika mitutu hao watakapokuwa wanawakaribisha Mashetani wekundu wa jiji la Manchester kwenye uwanja wa Emirates hapo
November 22.
Halikadharika Wenger amethibitisha maendeleo mazuri ya kiungo Jack Wilshere aliyekuwa anasumbuliwa na matatizo ya virusi na anatarajiwa kuwemo kwenye kikosi kitakacho wavaa Swansea, licha ya kuwa hali ya mlinzi Mfaransa Laurent Koscielny bado haijatengemaa.
Debuchy, Ospina na Ozil wote amewataja kuwa wanaendelea vizuri licha ya kusema kuwa hawatakuwemo kikosini kwa siku za hivi karibuni na matumaini ya kurejea kwao yakiwa baada ya michuano ya kimataifa kama ilivyo kwa Giroud.
Post a Comment