Kwa mujibu wa gazeti la London Evening Standard la huko nchini Uingereza, Austin anatajwa kuwa ndiye mchezaji aliyechangia kwa kiasi kikubwa kuisaidia QPR kurejea kwenye makali yake yaliyozoeleka kwenye Premier League msimu huu, ikishuhudiwa akifunga takribani magoli 6 kwenye michezo 10 aliyoichezea QPR.
Mshambuiaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kwa sasa alisajiliwa na matajiri hao wa QPR kutoka klabu ya Burnley kwa ada inayokisiwa kuwa ni paundi milioni 4 tu za Uingereza mnamo mwaka 2013 kwa mkataba wa miaka mitatu ambao ulikua ukimfanya mshambuliaji huyo ajinyakulia kitita cha paundi 28,000/= kila wiki.
Lakini QPR sasa imeamua kumpatia mkataba mpya utakaomfanya awepo kikosini hapo mpaka mnamo mwaka 2018 mkataba ambao utamfanya mchezaji huyo ajinyakulie kiasi cha paundi 50,000/= kila wiki ikiwa kama kifuta jasho chake.
Post a Comment