0
 

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Inter Milan ya nchini Italy Adriano amepandishwa kizimbani kwa kosa la kuwa na mahusiano na mmoja kati ya wafanyabiashara wakubwa  wa dawa za kulevya katika jiji la Rio de Janeiro.


Mwendesha mashitaka nchini Brazil ameiambia mahakama kuwa Adriano,mwenye umri wa miaka 32, mnamo mwaka 2007 alinunua pikipiki na kumpa mmoja kati ya wafanya biashara maarufu wa dawa za kulevya nchini humo.

 



Kwa mujibu wa muendeesha mashitaka huyo amedai kuwa pikipiki hiyo mara kadhaa imekua ikikamatwa na askari wa usalama barabarani nje na ndani ya jiji la Rio ikiwa imebeba dawa za kulevya na ilikamatwa wakati wa kampeni ya kitaifa za kuzuia usambaaji wa dawa hizo kampeni ambazo ziliendeeshwa na kikosi maalumu cha kupambana na hadarati nchini Brazil kinachofahamika kama Comando Vermelho (Red Command).

Kwenye mashitaka hayo yaliyosomwa na mwendeesha mashitaka huyo dhidi ya mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil pia aliiambia mahakama hiyo kuwa Adriano alipoinunua pikipiki hiyo aliisajili kwa jina la mama yake muuza unga huyo jambo ambalo linafanya waendelee kulitilia shaka zaidi dhumuni la kununuliwa kwa pikipiki hiyo.
  



Taarifa za mashitaka hayo zimekuja siku kadhaa mara maada ya kuarifiwa kuwa mchezaji huyo yuko kwenye hatua za mwishoni kujisajili na klabu ya ligi daraja la pili nchini Ufaransa ya Le Harve.

Mshambuliaji huyo aliyeifungia jumla ya magoli 71 katika michezo 174 klabu yake ya Inte Milan huenda akatakiwa kukitumikia kifungo cha miaka 10 jela endapo atakutwa na hatia.








Akizungumza na waandishi wa habari wakili wa mchezaji huyo amedai kuwa mteja wake amejikuta akiingia kwenye matatizo hayo kutokana na Pikipiki ambayo ilikua yake kununuliwa na mtu tofauti na aliyemuuzia Adriano bila ya yeye kufahamu na kuruhusu kufanyika biashara hiyo na aliongeza kudai kuwa hata saini iliyopo katika hati ya mauziano ya pikipiki hiyo ni yakughushi na sio ya mteja wake ( Adriano). Lakini akalishangaa jeshi hilo la polisi kumuweka kizuizini mteja wake kwa kosa hilo wakati tayari taarifa za wizi wa kuaminika wa pikipiki hiyo ziko mikononi mwao kutoka kwa Adriano.


 Prosecutors have ordered Adriano, pictured, to hand over his passport while the investigation continues 

Post a Comment

 
Top