Klabu ya Manchester inatarajiwa kuzikosa huduma za mlinzi wake wa kati anayekipiga raia wa Argentina Marcos Rojo mara baada ya kupata maumivu ya bega kwenye mchezo wa mahasimu wao wa mji mmoja klabu ya Manchester City.
Meneja
wa klabu ya Manchester United Mholanzi Louis
van Gaal amethibitisha maumivu ya mlinzi wake wa kati raia wa Argentina
Marcos Rojo ambaye amejitonesha maumivu bega lake kwenye mchezo ambao
timu yake ilipoteza kwa goli 1-0
dhidi ya Manchester City kwenye dimba la Etihad Stadium.
Rojo
alitolewa mapema kipindi cha pili na kuwekewa mtungi wa gesi ya
oksijeni mara baada ya kupatwa na maumivu hayo ya bega kwenye mchezo
huo.
Muajentina
huyo sasa ataungana na majeruhi wengine ndani ya klabu hiyo wakiwemo
Rafael na Phil Jones huku Chris Smalling akiwa anatakiwa kutumikia
adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata kwenye mchezo huo dhidi ya
manchester City ikishuhudiwa United ikiangukia pua dhidi ya mahasimu
wake hao wa mji mmoja.
"Ameumia bega, limetoka kwenye sehemu yake, hivyo huwezi kujua ni kwa muda gani atakua nje ya uwanja," Van Gaal alikiambia kituo cha televisheni cha Sky Sports cha nchini Uingereza. "Tuanatakiwa kusubiri mpaka kesho lakini kutokana na hali ya mambo ilivyo hataweza kucheza dhidi ya Crystal Palace."

Post a Comment