Katika kile kinachoonekana kama ni kujiwekea kumbukumbu ya nguvu kutokana na madaraka yake ya unahodha aliyoyatumikia kwa miaka kadhaa sasa, nahodha wa klabu ya Chelsea Muingereza John Terry ametuma picha kwenye mtanadao wa Instagram kuonesha beji zake zote za unahodha alizowahi kuzivaa kwenye michezo mbalimbali kwa vilabu mbali mbali na timu yake ya Taifa.
Terry ameandika kupitia mtandao huo kuwa: 'Nimehifadhi vitambaa vyangu vyote vya unahodha kwa miaka mingi sasa na ninatarajia kuongeza zaidi kwenye mchakato wangu huo wa kuzikusanya beji hizo nikiwa mwenye kujivuna na najiona ni mwenye kuheshimika zaidi"
Ukiachilia mbali na vitambaa hivyo vya unahodha lakini katika kipindi cha miaka 10 ya unahodha wa klabu ya Chelsea pia vipo vingine alivyovitwaa akiwa kama nahodha wa timu ya Taifa ya Uingereza The three Lions.
Terry, mwenye umri wa miaka 33 sasa ndiye nahodha mwenye mafanikio zaidi pale Stamford Bridge, akiwa ameshinda vikombe vitatu vya ligi kuu ya Uingereza, Vinne vya FA, Viwili vya kombe la ligi (Capital One) na kimoja cha UEFA
Champions League akiwa na Chelsea.
Post a Comment