0
De Gea 'rejects new Man United contract and closes on Madrid transfer'
David De Gea ameripotiwa kugoma kufanya mazungumzo ya mkataba mpya na klabu yake ya Manchester United ikitajwa kuwa ni njia moja wapo ya kuhakikisha mpango wake wa kutua klabu ya Real Madrid unatimia.

De Gea ametajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaowindwa na klabu ya Real Madrid katika siku za hivi karibuni akionekana kuwa ndio mrithi muafaka wa mlinda mlango namba moja wa klabu hiyo ya Real Madrid Iker Casillas.

United wanasemekana kutaka kufungua mazungumzo yenye lengo la kumungeza mkataba na mlinda mlango huyo lakini taarifa zinadai kuwa De Gea amegomea mazungumzo ya mkataba huo ikiwa ni dalili waziwazi ya kutaka kujiunga na klabu ya Real Madrid.

Mashetani wekundu hawako tayari kuona mchezaji huyo akiondoka ndani ya klabu hiyo hivyo wameahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa mlinda mlango huyo anabakia klabuni hapo.

Post a Comment

 
Top