0
DIEGO SIMEONE anatajwa kuwa ndiye chaguo namba moja la klabu ya mancheste City ambayo siku za hivi karibuni imetajwa kuwa na nia ya kutaka kumtimua meneja wake wa sasa Manuel Pellegrini. Pellegrini anaonekana kukalia kuti kavu kutokana na matokeo yasiyo eleweka ya mabingwa hao watetezi wal ligi kuu nchini Uingereza.

Taarifa za ndani ya klabu hiyo zinadai kuwa mabosi wa klabu hiyo tayari wameshaanza kufanya mchakato wa chinichini kumtafuta mrithi wa kocha huyo ambaye rasmi sasa imefahamika kuwa mkataba wake unatarajiwa kufanyiwa mapitio mnamo mwishoni mwa msimu huu.
 
Bosi wa klabu ya Atletico Madrid ambaye aliisaidi timu hiyo kunyakua ubingwa wa La Liga msimu uliopita huku akishuhudiwa akipokonywa tonge mdomoni kwenye mchezo wa fainali ya UEFA Champions League kwenye dakika za mwisho dhidi ya mahasimu wake wa mji mmoja Real Madrid ndio anatajwa kama mtu muafaka wa kuchukua nafasi ya kocha huyo raia wa Chile. 


Pep Guardiola amekua akitajwa sana na wadadisi wa masuala ya soka kuwa ni mtu sahihi kukalia kiti hicho lakini pia mahusiano yake na mabosi wa klabu ya Manchester City Ferran Soriano na Txiki Begiristain ambao tayari amekwishawahi fanya nao kazi kwenye klabu ya Barcelona kilikua ni moja kati ya kitu kilichofanya watu wengi waamini kuwa kocha huyo atatua Man City.


Tatizo lililopo kwa bosi huyu wa klabu ya Bayern Munich ni kuwa kwa sasa ndiye kocha anayevuta mkwanja mwingi sana kutoka kwa mwajiri wake kuliko makocha wengine wote Duniani akiwa anaweka kibindoni kiasi cha paundi milioni 12.5 kwa mwaka, kitu ambacho mabosi hao wa klabu ya Man City wamesema hawataki kukiona kikifanyika kwa sasa kutokana na mfumo waliojiwekea wa kubana matumizi.

Kutokana na maamuzi hayo ya kuamua kubana matumizi kuwa ndio mpango mkakati wa klabu ya Manchester City kwa sasa mabosi hao wanamuona Simeone kama ndiye mrithi muafaka mara baada ya Pellegrini kufungashiwa vilago ndani ya Etihad.

Post a Comment

 
Top