Klabu ya Real Madrid imeanza kuingiwa na mchecheto kuwa huenda klabu ya Chelsea ikatibua mipango yao inayokwenda vivuri ya kutaka kumsajili kiungo Mjerumani anayekipiga kwenye klabu ay Borussia Dortmund Marco Reus.
Marco Reus anatajwa kutaka kuondoka kwenye klabu yake ya sasa ya Dortmund na mpaka sasa vilabu vya Bayern Munich. Arsena, Chelsea, Manchester United na Real Madrid vimeonesha nia ya dhahiri ya kutaka kumnasa kiungo huyo mahili.
Nia ya vilabu hivi kuanza kupigana vikumbo vya kutaka kuwania saini ya kiungo huyo inachagizwa na kitendo cha mchezaji huyo kukataa kuongeza mkataba na klabu yake ya BvB na hivyo kufungua milango kwa mwenye kisu kikali aweze kuinasa saini ya kiungo huyo mahiri.
Kwenye mkataba wake unaoelekea ukingoni kuna kipengele kinachotaka timu itakayokuja na kiasi cha paundi milioni 19.7 kumnyakua mchezaji huyo na Real Madrid inatajwa kuwa tayari kulipa kiasi hicho cha pesa ili kuinasa saini yake.
Hofu ya Real inakuja kutokana na nia ya klabu ya Borussia Dortmund ya kutaka kumsajili kiungo Andre Schrrle kutoka klabu ya Chelsea na hivyo wanahisi huenda mchezaji huyo akatumika kama chambo katika kuhakikisha dili hilo linatimia kwa kumtumia mchezaji huyo kama chambo na sehemu ya makubaliano ya dili hilo kukamilika.
Post a Comment