Mshambuliaji huyo raia wa Ubelgiji anayetajwa kuwa na asili ya Kenya anakipiga kwa mkopo wa muda mrefu kwenye klabu hiyo ya Lille ya nchini Ufaransa.
Origi amesema yeye ni mchezaji na yuko tayari kucheza kwenye klabu yoyote ile na kama timu yake itakua inataka kumuuza mnamo mwezi wa January basi chaguo lake litakua klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza.
"Natamani kuendelea kubakia hapa kwani ni moja kati ya sehemu ambayo nafurahia sana maisha yangu ya kiuchezaji na natamani kubakia hapa kwa muda mrefu zaidi lakini hilo litabakia kuwa ni makubalianao baiana ya vilabu vyenyewe."
"Ni mchezaji gani asiyetaka au kutamani kuchezea kwenye EPl? ni moja kati ya ligi kubwa, maarufu na yenye mvuto mkubwa sana hivyo kama ikitokea nafasi ya kwenda huko nitaifurahia na kuipokea kwa mikono miwili lakini Liverpool ndilo chaguo langu la mwanzo."
Post a Comment