0
Why Gonzalo Higuain could be the man to save Liverpool's season
Siku za hivi karibuni kumeibuka tetesi kuwa klabu ya Napoli ya huko nchini Italy imeanza kumtafuta mbadala wa kwenda kuziba pengo la mshambuliaji anayetajwa kutaka kujiunga na klabu ya Liverpool,Gonzalo Higuain.

 Balotelli was on the losing side on Saturday as Liverpool went down 3-1 to West Ham
Taarifa zinadai kuwa Muargentina huyo anaonekana kutoyafurahia maisha ya ujumla katika jiji la Naples hivyo kuamua kuangalia wapi ambapo atakwenda kuishi maisha ya furaha na Liverpool inatajwa kuwa moja kati ya sehemu hizo.

 Lambert grins as he walks back to his seat, the 32-year-old appears to see the funny side of the situation
Liverpool kwa siku za hivi karibuni imeonekana kusaka saini ya mshamnuliaji wa kiwango cha juu Duniani ili kuja kuziba pengo la mshambuliaji Luis Suarez aliyetimukia kwa Magalaktiko wa Real Madrid. 

 Lallana (left) has made a reasonable start since leaving Southampton but a £23.7m fee demands more
Lakini klabu hiyo inaonekana kuumiza kichwa zaidi kutokana na kutokipata kile walichokuwa wanakitarajia kutoka kwa Mario Barotel, Lalana na Rickie Lambert ambao wote wameshindwa kuonesha cheche zao ndani ya anfield.

 Philippe Coutinho (top) doesn't look impressed with Raheem Sterling's carrying on during the training session
Ukweli ni kwamba kwa sasa Livepool wanayamiss sana magoli ya Luis Suarez lakini pia majeraha ya mara kwa mara ya mshambuliaji wao tegemeo Daniel Sturridge yanawachanganya mno na zaidi ya yote ni juu ya lile nililolisema awali ni kitendo cha Mario Balotelli na Rickie Lambert kushindwa kumpa furaha meneja Brendan Rodgers. 

 Rodgers is set to rest Gerrard against Real Madrid and start Henderson as captain for Liverpool on Tuesday
Liverpool inamhitaji mshambuliaji wa kalba ya Higuain kwani tayari akiwa kwenye Seria A ameonesha kuwa yeye ni mmoja kati ya wakali wa mabao Duniani na hivyo huenda akawa tiba mujarabu kwa maradhi wanayougua Liverpool kwa sasa.

 Gerrard (centre) surrounded by Mario Balotelli (to his right) and his Liverpool team-mates in Madrid
Liverpool inamhitaji mshambuliaji wa kiwango cha Higuain ili kuinusuru nafasi yao ya kucheza michuano ya UEFA Champions League kwa msimu ujao vinginevyo watarejea tena kenye aibu ya miaka kadhaa iliyopita ya kukaa kwenye Luninga zao wakiwatazama wenzao wakipambana na kuingiza mamilioni ya pesa kutokana na ushiriki wao kwenye mashindao hayo makubwa barani Ulaya.

Post a Comment

 
Top