0
Klabu ya Manchester United inaonekana kuwa msitari wa mbele katia kuhakikisha inainasa saini ya mlinzi Mfaransa anayekipiga kwenye klabu ya Athletic Bilbao, Aymeric Laporte.

Laporte kwa siku za hivi karibuni ameripotiwa kusakwa kwa udi na uvumba na vilabu vya Chelsea na Arsenal ambavyo vyote vina nia ya kutaka kuimarisha safu zao za Ulinzi.

Tayari klabu ya Manchester United inatajwa kuwa tayari imekwishatua nchini Hispania kwenye klabu ya Athletic Bilbao na kufanya maulizo ya ada sahihi ambayo inaweza kumng'oa mchezaji huyo kwenye klabu yake hiyo.

Klabu ya Manchester United inatajwa kuwa ni moja kati ya vilabu ambavyo sehemu yake ya ulinzi haiko sawasawa na hivyo inaonekana kuwa katika harakati nzito za kutaka kuimarisha safu yake hiyo.

Heading for Bayern? Laporte (right) could be set to swap the Spanish top flight for the Bundesliga
Na katika kuhakikisha mkakati wake huo unakamilika, tayari kigogo mwenye dhamana ya kushughulikia masula ya usajiri ndani ya Old Trafford ambaye pia ni makamu mwenyekiti wao Ed Woodward amekwishatua nchini Hispania ikiwa ni moja kati ya hatua ya kutatua matatizo yao ya ulinzi yanayowakabili kwa sasa.

Meneja wa klabu ya Manchester United Luis Van Gaal ameorodhesha wachezaji kadhaa anaotamani kufanya nao kazi ndani ya timu hiyo Mfaransa  Laporte akiwa mmoja wao.

Taarifa zinadai kuwa kipengele kinachoruhusu kuvunjwa kwa mkataba wa mchezaji huyo ni paundi za Uingereza milioni 32 na hivyo kazi inabakia kwa Man Utd na vilabu vingine vinavyomuhitaji mchezaji huyo kutimiza matakwa hayo ya mkataba halikadhalika matakwa binafsi ya mchezaji ili kukamilisha dili hilo.

Post a Comment

 
Top