Shirika la utangazaji la nchini Uingereza BBC limeitaja orodha ya wachezaji kadhaa wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika hapo jana lakini wote wakiwa ni wale wanaokipiga kwenye ligi mbalimbali barani Ulaya.Yaya Toure ametajwa kwenye orodha hiyo ikiwa ni mara ya sita mfululizo, lakininpia kwenye orodha hiyo ndefu ya BBC wako wachezaji maarufu kama Pierre-Emerick Aubameyang, Yacine Brahimi, Vincent Enyeama na Yao Gervinho anayetajwa na wadadisi wengi wa masuala ya soka kuwa ndiye mtu muafaka kwa tuzo hiyo msimu huu.
Tuzo hizo zinazotarajiwa kutolewa mnamo January 8, mwaka 2015 zinaonekana kuwa na ushindani mkubwa kutokana na aina ya wachezaji waliojumuishwa kwenye shindano hilo na sifa zao.Jumla ya wachezaji 25 wametajwa kuwania tuzo hiyo akiwemo Ahmed Musa ambaye kwa sasa anafanya vyema akiwa na klabu yake ya CSKA Moscow ya nchini Urusi ambaye aliiongoza vyema timu yake hiyo kuwafumua Manchester City kwenye mchezo wa makundi ya michuano ya UEFA Champions League,Lakini yumo pia na Mehdi Benatia mchezaji pekee wa kiafrika aliyenufaika na uhamisho wake wa kujiunga na klabu ya Bayern Munich, Lakini pia katika orodha hiyo wamo pia wachezaji maarufu wanaotoka katika bara hili kama vile; Emmanuel Adebayor, Stephane Mbia,
Islam Slimani na Asamoah Gyan.
Washindi waliopita wa tuzo za BBC za mchezaji bora wa Afrika:
2013 -
Yaya Toure
(Manchester City & Ivory Coast)
2012 -
Chris Katongo
(Henan Construction & Zambia)
2011 -
Andre Ayew
(Marseille & Ghana)
2010 -
Asamoah Gyan
(Sunderland & Ghana)
2009 -
Didier Drogba
(Chelsea & Ivory Coast)
2008 -
Mohamed Aboutrika
(Al Ahly & Egypt)
2007 -
Emmanuel Adebayor
(Arsenal & Togo)
2006 -
Michael Essien
(Chelsea & Ghana)
2005 -
Mohamed Barakat
(Al Ahly & Egypt)
2004 -
Jay-Jay Okocha
(Bolton & Nigeria)
2003 -
Jay-Jay Okocha
(Bolton & Nigeria)
2002 -
El Hadji Diouf
(Liverpool & Senegal)
2001 -
Sammy Kuffour
(Bayern Munich & Ghana)
2000 -
Patrick Mboma
(Parma & Cameroon)
Post a Comment