Mabosi wa klabu ya Manchester United watasafiri kwenda jijini Rome nchini Italy wakiwa na kiasi cha paundi milioni 30 kibindoni kwenda kumnasa kiungo wa klabu ya AS Roma ya nchini humo Kevin Strootman siku ambayo atakua anarejea kutoka kwenye majeruhi yaliyomfanya kuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu kidogo.
Kiungo mholanzi anayekipiga kwenye klabu ya AS Roma amekua akifuatiliwa kwa ukaribu sna na mabosi wa klabu ya Manchester United na kwa kipindi kirefu sasa kuanzia mwezi March alikua yuko nje ya uwanja kutokana na kuuguza jeraha la kifundo cha mguu alilolipata takribani miezi minane iliyopita wakati klabu yake ilipokua ikikipiga dhidi ya klabu ya Napoli ya nchini Italy.
Mmiliki wa klabu ya Roma James Pallotta ameendelea kusisitiza kuwa kiungo huyo hauzwi kwa timu yoyote ile isipokuwa itakayokuwa imefikia ada ya uhamisho wa paundi milioni 100. Lakini taarifa zinadai kuwa kiungo huyo wa zamani wa klabu ya PSV Eindhovenya nchini Uholanzi ameonesha nia ya kutaka kutua Old Traford ili akaungane na kocha wake wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi Louis Van Gaal kwa mara nyingine tena.
Na katika kuhakikisha kuwa maamuzi yake hayo ya kujiunga na United yanatimia Strootman aliamua kuachana na wakala wake wa muda mrefu Chiel Dekker na kusaini makubaliano na wakala mpya anayefahamika kwa jina la Kees Vos ambaye ndiye aliyefanikisha dili la kumhamisha mshambuliaji Robin van Persie kutoka klabu ya Arsenal kwenda Manchester United mnamo mwaka 2012.
Tayari meneja Luis Van Gaal amekwisha ambiwa kuwa klabu yake ina pesa za kutosha kufanya manunuzi makubwa ya wachezaji wa kiwango cha juu duniani lengo likiwa ni kumpa uwanja mpana wa kuwapata wachezaji watakaoendana na mfumo wake.
Post a Comment