Kikundi cha mashabiki wa klabu ya
Crystal Palace kinachofahamika kama Holmesdale Fanatics kimewasilisha maoni yao ya kutotaka ligi kuu ya nchini Uingereza kutochezwa nje ya Uingereza kama vile ambavyo watendaji wakuu wa chama cha soka nchini humo walipendekeza siku kadhaa zilizopita kwamba katika msimu mmoja kuwe na michezo takribani 38 itakayokua inachezwa nje ya ardhi ya Uingereza.
Mashabiki hao waliokuwepo uwanjani hapo waliliwasilisha mawazo yao hayokwenye mchezo wao wa ligi ambao pia ulikua ukirushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Sky. Bango la mashabiki hao lilikua likisomeka 'No to the 38th game abroad - English games on English soil". Wakiwa wanamaana ya kukataa kabisa michezo hiyo 38 kuchezwa nje ya nchi yao wakitaka michezo yao ichezwe kwenye ardhi yao wenyewe.
Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi kuu nchini humo Richard Scudamore alihudhuria mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Selhurst
Park ambayo ndiyo inayoaminika kuwa ndio sababu kuu ya kundi hilo la mashabiki kuwasilisha maoni yao kupitia ujumbe huo wa maandishi.
Ikumbukwe kuwa mwezi uliopita mashabiki haohao walifanya tena jambo linalofanana na hili pale timu yao ilipokua ikikipiga dhidi ya timu ya Chelsea lililokuwa likisomeka 'Roman's dirty money is a disgrace that has plagued our game'. Wakiwa wanamaanisha pesa haramu (zilizopatikana kutokana na biashara ambayo sio halali) ni aibu inayoleta madhara ndani ya soka lao.
Mashabiki hawa hawakuishia hapo tu bali ikumbukwe kuwa mashabiki hawahawa waliandamana kupinga kitendo cha kituo cha televisheni cha Sky Sports kuonesha na kuripoti moja kwa moja masuala ya uasjili yanavyoendelea katika siku ya mwisho ya usajiri.
Post a Comment