Klabu ya Arsenal inaarifiwa kujiandaa kutuma ofa ya paundi milioni 7 kwenda kwa majirani zao wa jiji la London klabu ya Chelsea ili kumnasa mlinda mlango anayeonekana kuwa hana tija sana kwa sasa ndani ya klabu hiyo Petr Cech.
Kwa mujibu wa gazeti la The Sun,
limeandika kuwa bosi wa The Gunners mfaransa Arsene Wenger anajiandaa kufanya hivyo kwa kuwa kocha wa klabu ya chelsea Mreno Jose
Mourinho anajiandaa kumuuza mkongwe huyo itakapofika mwezi January na katika mpango wake huo kamwe hatakua na mipaka kuwa amuuze kwa klabu inayoshiriki ligi gani na katika nchi gani.
Taarifa zinadai kuwa Wenger anauhakika na kuvishinda vilabu vya Liverpool, Manchester United, Paris Saint-Germain na
Real Madrid katika mbio za kumsajili mlinda mlango huyo sababu kubwa ya kujivuna kwake ikiwa ni familia ya mlinda mlango huyo ambayo inatajwa kuwa tayari imekwishaweka mizizi jijini London ambayo ndiyo masikani ya vilabu vya Chelsea na Arsenal.
Arsenal inasemekena kuwa iko tayari kutoa kiasi cha paundi 100,000 ya mshahara wa mchezaji huyo ikiwa ni kiasi sawa anachokipata pia ndani ya klabu yake ya sasa ya Chelsea na inauhakika wa kupata pesa hizo kwani kwenye bajeti yake ana takribani kiasi cha paundi 20 elfu kwaajili ya kufanya manunuzi mnamo mwezi January.
Mourinho anatajwa kuwa na nia ya kutaka kumpa Peter Cech nafasi ya kutafuta mahali anapodhania kuwa atapata nafasi ya kucheza kwani kwa sasa kiwango chake hakimfikii mlinda mlango wa sasa wa klabu hiyo Thibaut
Courtois.
Post a Comment