0
Arsenal close on £26m Pedro as he drops HUGE Barca exit hint
Arsenal iko katika hatua nzuri ya kuhakikisha inakamilisha dili la uhamisho la paundi milioni 26 ili kumnasa mshambuliaji wa pembeni wa klabu ya Barcelona Pedro Rodriguez mara baada ya mchezaji huyo kuvunja ukimya kuhusiana na hali ya mambo inavyoendelea ndani ya klabu hiyo ya Wakatalunya. 

Bosi wa The Gunners Arsene Wenger amekua akimuhitaji mchezaji huyo kwa muda mrefu sasa na wadadisi wa masuala ya soka wanadai kuwa ni takribani vipindi vitatu tofauti Mfaransa huyo ameonesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliji huyo bila ya mafanikio.

Uwezekano wa Arsenal kumsajili msahmbuliaji huyo unakuja kutokana na Pedro mwenyewe kutanabahisha kuwa yeye kama mchezaji hajisikii vizuri sana kuona akiwa hapati nafasi ya kucheza ndani ya timu hiyo wakati uwezo wake unamruhusu kufanya hivyo.

Katika mazungumzo yake hayo mshambuliaji huyo alisisitiza kuwa bado ataendelea kupambana kuonesha kiwango cha juu ndani ya klabu hiyo mpaka mwisho lakini akadai endapo hakutakuwa na mabadiliko basi atatafuta njia nyingine mbadala na kuondoka ndani ya klabu hiyo ndio litakua suluhisho pekee lililosalia.

Taarifa zinadai kuwa klabu ya Arsenal ilipanga kupeleka kitita cha paundi milioni 26 kwa wakatalunya hao ili kuhakikisha wanamnasa mshambuliaji huyo wa pembeni wa klabu ya Barcelona.

Post a Comment

 
Top