Mshambuliaji wa klabu ya Napoli na timu ya taifa ya Italia Lorenzo Insigne anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi sita kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu aliyoyapata siku ya jana Jumapili wakati timu hiyo ilipopata ushindi mwembamba wa goli 1:0 dhidi ya Fiorentina.
Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Napoli zinadai kuwa mchezaji huyo atalazimika kufanyiwa upasuaji kwenye jeraha lake hilo, Upasuaji uliofanyika hii leo hukohuko nchini Italia.
Akizungumza na waandishi wa habari kuthibitisha majeraha hayo yanayomkabili mshambuliaji huyo ambaye tayari alikwisha jumuishwa kwenye kikosi cha meneja mpya wa timu ya taifa ya Italia Antonio Conte, meneja wa klabu ya Napoli Rafa Benitez amesema kumkosa mchezaji wa kalba ya Insigne tena kwa kipindi kirefu si kitu kizuri sana kwani kwa namna moja au nyingine kunavuruga mipango ya mbio za ubingwa.
Katika kuhakikisha kuwa kikosi chake kinakua na makali yale yale meneja wa timu ya taifa ya Italia Antonio Conte amemjumuisha kikosini mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid Alessio Cerci kwaajili ya mchezo ujao wa kufuzu kwa michuano ya Ulaya ya mwaka 2016 na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Albania.
Post a Comment