0
Barcelona defender Gerard Pique during a training session  in Amsterdam on Tuesday

Vilabu vitatu vya Premier League vya Arsenal, Chelsea na Manchester United vimeanza kupigana vikumbo kuwania saini ya mlinzi wa klabu ya Barcelona ambaye anaonekana kama kuanza kufungiwa vilago ndani ya klabu yake ya Bacelona Gerard Pique ambaye usiku wa jana aliachwa kwenye kikosi cha klabu ya Barcelona kilichokua kikiminyana na klabu ya Ajax ya huko nchini Uholanzi. 

 Pique was left in the stands for the team's last match against Celta Vigo on Saturday

Pique aliachwa nje ya kikosi kilichoanza kwenye mchezo huo ukiwa ni mchezo wake wa pili mfululizo kuwekwa nje na taarifa zinadai kuwa vilabu hivyo vitatu vya nchini Uingereza vimetuma ofa kwa nyakati tofauti kutaka kumnyakua mchezaji huyo.

 

Kwenye michezo yote miwili aliyowekwa nje mchezaji Marc Bartra alicheza kama mlinzi wa kati pamoja na mkongwe Javier Mascherano, na maamuzi ya meneja wa klabu ya Barcelona Luis Enrique kuamua kumuweka Pique kwenye benchi kwenye mchezo ambao klabu ya Barcelona iliibuka na ushindi wa mabao 2:0 kimeyafanya magazeti mengi ya nchini Uhispania kuanza kudadisi juu ya mustakabali wa mchezaji huyo ndani ya Nou Camp.

Post a Comment

 
Top