Klabu ya Manchester United rasmi imefungua mazungumzo na klabu ya Sporting Lisbon kujadili suala la winga Mreno Luis Nani kurejea tena kwenye timu hiyo mnamo mwezi January mwakani.
Nani alijiunga na klabu ya Sporting Lisbon wiki 12 zilizopita kwa mkopo wa muda mrefu mpaka mwishoni mwa msimu huu lakini uwezo wake wa siku za karibuni umelivutia sana benchi la ufundi la klabu hiyo na hivyo kuanza kuangalia uwezekano wa kumrejesha tena kikosini.
Ripoti kutoka nchini Uingereza zinadai kuwa klabu ya Manchester United wanataka kumrejesha kikosini mapema kabla ya muda wa makubalianao kutokana na hali ilivyo sasa ndani ya klabu hiyo na pia uwezo uliooneshwa na Luis Nani siku za hivi karibuni.
United wanauhakika kumrejesha mchezaji huyo kikosini mapema iwezekanavyo kutokana na ukweli kwamba klabu ya Sporting Lisbon haimlipi mshahara Luis Nani na pia hawajailipa United kiasi chochote kile cha pesa kwaajili ya malipo ya ada ya uhamisho wa mkopo wa mchezaji huyo hivyo United watakua wakisubiri huruma ya mchezaji mwenyewe kwani imefahamika kuwa ndiye atakayekuwa na kauli ya mwisho katika makubaliano haya mapya.
Nani amefunga magoli sita katika michezo 13 aliyoichezea klabu yake ya sasa ya Sporting na akitoa takribani pasi 7 za mwisho kwenye michezo hiyo 13.
Post a Comment