0
Podolski has had to deal with a bit-part Arsenal role of late, mainly warming the bench at the EmiratesMshambuliaji raia wa Ujerumani anayekipiga kwenyea klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza Lukas Poldoski jana kwa mara nyingine tena amembwatukia meneja wa timu yakae Mfaransa Arsene Wenger kutokana na aina ya upangaji wake aliouita wenye upendeleo wa kikosi hicho licha ya ukweli kwamba klabu hiyo ina wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu wenye uwezo wa kuwapa raha mashabiki wa klabu hiyo.

Podolski in training at London Colney this week, before Arsenal's Champions League tie

Akizungumza mara baada ya timu yake ya taifa ya Ujerumani kupata ushindi wa jumla ya magoli  4-0 dhidi ya timu ya taifa ya Gibraltar kwenye mchezo wa kampeni za kuwania kufuzu kwa michuano ya Ulaya mwaka 2016, Poldoski amemlaumu meneja wake huyo kwa kushindwa kumpa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha klabu ya Arsenal licha ya kuwa katika kiwango kizuri kwa sasa.

 Podolski (centre) alongside Alexis Sanchez walk out for the warm-up at the Emirates on Wednesday
"Nimetumia takribani miezi minne iliyopita kuhakikisha kuwa ninajiweka vizuri ili kuingia kwenye ushindani wa namba klabuni hapa lakini mwalimu amekua haniamini bila ya sababu yoyote ile. mimi kama mchezaji siku zote natamani kucheza mpira maana ndio kazi yangu, ninauwezo nadhani anachotakiwa kukifanya ni kunipa nafasi ili niudhihirishie ulimwengu ubora wangu."

Podolski in training at London Colney this week, before Arsenal's Champions League tie
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari hao Poldoski amesita kukanusha moja kwa moja kama ataendelea kubakia ndani ya klabu ya Arsenal au ataondoka maana kwa jinsi hali ya mambo ilivyo hivi sasa kwenye tasnia la mpira lolote linawezekana.

Post a Comment

 
Top