0
Liverpool to make shock £25m bid for Chelsea flop Schurrle
Klabu ya Liverpool imetangaza rasmi nia ya kutaka kumsajili kiungo mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Andre Schurrle kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 25 kwenye dirisha la usajili la mwzi January.

Kiungo huyo raia wa Ujerumani tayari amekwisha ambiwa na mabosi wa pale darajani (Stamford Bridge) kuwa anaweza kuenda atakako kwenye kipindi hicho cha usajiri wa dirisha dogo la mwezi January baada ya kushindwa kumvutia meneja wa timu hiyo Jose Mourinho. 

Taarifa zinadai kuwa Liverpool tayari inajiandaa kuweka mezani mzigo huo wa paundi milioni 25 ili kunasa saini ya mshambuliaji huyo ambaye tayarti inasemekana klabu ya Tottenham nayo imekuwa ikimfuatilia kwa ukaribu pamoja na vilabu kadhaa vya nchiniUhispania.

Klabu ya Borussia Dortmund nayo tayari imekwisha onesha nia ya kutaka kumsajili kiungo huyo ikimtazama kama mbadala wa kiungo wake wa sasa aliyegoma kuongeza mkataba na timu hiyo Marco Reus anayewindwa pia na vilabu kadhaa vya barani Ulaya.
 
Schurrle alijiunga na Chelsea kutoka klabu ya Bayer Leverkusen mnamo mwaka 2013 kwa ada ya uhamisho ya paundi za Uingereza kiasi cha paundi milioni 18  ameifungia Chelsea magoli 11 katika michezo 54 aliyokwishacheza.

Post a Comment

 
Top