Mara baada ya kupata ushimdi wa jumla ya 3-1 dhidi ya timu ya taifa ya Slovenia kwenye uwanja wa Wembley hapo jana washabiki wa timu ya Taifa ya Uingereza wamempachika jina la "Wele" wakimfananisha na gwiji la soka la nchini Brazil Pele.
Mara baada ya mchezo huo ambao welbeck aliifungia magoli mawili timu yake hiyo ya taifa wako watu wengine waliomfananisha mchezaji huyo na mwokozi na kutupia picha zinazomuonesha mchezaji huyo akiwa amevalia mavazi matakatifu.
Wengine wamekwenda mbali zaidi kwa kumfananisha mchezaji huyo na mtoto wa familia ya kifalme kutokana na raha waliyopewa na mchezaji huyo mara baada ya kuifungia timu hiyo ya taifa jumla ya magoli mawili.
Mashabiki wa timu ya taifa ya Uingereza wanaonekana kujikuta wakiingia kwenye furaha iliyopitiliza kutokana na ari inayooneshwa na timu yao hiyo kwani mara ya mwisho timu hiyo iliwahuzunisha sana mashabiki wake kwenye michuano ya kombe la Dunia walipotolewa kwenye hatua za awali za michuano hiyo dhidi ya timu ya taifa ya Italia.
Post a Comment