Barcelona huenda ikamwajiri kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho kama kocha mpya wa klabu hiyo iwapo tu Joan Laporta atashinda nafasi ya Uraisi wa klabu hiyo kwenye uchaguzi ujao wa klabu hiyo.
Mourinho ameibuka kuwa agenda kuu kwenye kampeni ya uraisi wa Joan Laporta kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa nafasi ya uraisi wa klabu hiyo
Mreno huyo ameshindwa kuzizuia hisia zake za mapenzi yake kwa klabu ya Barcelona mara kadhaa hata alipokuwa akiiongoza klabu mahasimu wakubwa wa klabu ya Barcelona ya Reala Madrid.
Laporta ameeleza mipango yake hiyo kwenye wakati ambao meneja wa sasa wa klabu hiyo Luis Enrique anaonekana kukalia kuti kavu ndani ya klabu hiyo kutokana na mwenendo usioeleweka wa klabu hiyo kwa sasa.
Post a Comment