Klabu ya Manchester
United imempatia miezi mitano mshambuliaji wake anayekipiga kwa mkopo kwenye klabu hiyo Radamel Falcao ikiwa ni mpaka mwezi wa April mwakani ili kujihakikishia kupewa mkataba wa kudumu na mashetani wekundu hao.
Falcao alirejea jana kwa mara ya kwanza ikiwa ni wiki 6 tangu awe nje ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na maumivu akimpokea Robin van Persie
mnamo dakika ya 70 ya mchezo ambao klabu ya Manchester United ilipata ushindi wa jumla ya magoli 3:0 dhidi ya Hull City.
Kalbu ya manchester United na AS Monaco zilifikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji huyo kwa ada ya paundi milioni 6 ikiwa ni ada ya usajili wa mkopo wa muda mrefu na endapo mshambuliaji huyo ataonesha uwezo mkubwa basi atapatiwa mkataba wa kudumu na klabu hiyo ambao utaifanya klabu ya monaco ijinyakulie kitita cha paundi milioni 50 ikiwa kama ada ya uhamisho.
Post a Comment