0
Man United 'offer Ancelotti £270,000-a-week deal to replace Van Gaal'
Klabu ya Manchester United imempa ofa nono meneja wa sasa wa klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania Carlo Ancelotti ili kumshawishi kuja kuchukua nafasi ya meneja wa sasa wa mashetani wekundu hao Luis Van Gaal.

Taarifa zinadai kuwa mashetani wekudu hao wako tayari kumpatia mkataba mnono wa mshahara wa kiasi cha paundi 270,000 kwa wiki ikiwa ni ishara tosha ya klabu hiyo kuanza kupoteza imani na meneja wake wa sasa Mholanzi Louis van Gaal.

Ancelotti ameliambia gazeti moja la michezo la nchini Hispania kuwa kwa nyakati mbili tofauti amezikataa ofa za kuifundisha klabu ya Manchester United ikidai mara ya kwanza kuwa mrithi wa Sir Alex Ferguson na mara ya pili mara baada ya kutimuliwa kwa meneja David Moyes.

Klabu ya Manchester United inamuona Mholanzi Luis Van Gaal kuwa si mtu sahihi katika mpango wao wa kuirejesha timu hiyo kwenye makali yake ya kawaida kutokana na mwenendo wa kusuasua wa timu hiyo kwa sasa licha ya kufanya matumizi makubwa ya kuwajumuisha kikosini wachezaji kadhaa wenye majina makubwa kikosini humo.

Hivyo basi klabu hiyo inamtazama Ancelotti kama mtu muafaka kuja kuirejesha United kwenye kiwango chake cha kuw moja kati ya timu tishio ulimwenguni.

Post a Comment

 
Top