Klabu ya Arsenal inakaribia kumsajili kiungo Mbrazil Romulo anayekipiga kwenye klabu ya Spartak Moscow ya nchini Urusi.
Romulo aliyehusishwa na kujiunga na washika mitutu hao tangu usajili wa majira ya joto yaliyopita anatajwa kuwa katika hatua za mwishomwisho za kutaka kujiunga na Arsenal ambayo iko katika hatua nzuri ya mazungumzo na klabu yake ili kuinasa saini ya kiungo huyo mahiri.
Taarifa zinadai kuwa klabu ya Arsenal inataka kuhakikisha kuwa inalikamilisha dili hilo kabla ya kesho Jumatatu lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa mchezaji huyo asije akanaswa na vilabu kadhaa vya nchini kwao Brazil vinavyoonekana kuwa na dhamira ya kutaka kumrejesha nyumbani mchezaji huyo.
Post a Comment