0

Hat-trick hero Muller shares a laugh with team-mate Xabi Alonso (left) during their away game 

Wakala wa FIFA mwenye nguvu sana katika masuala ya uwakala Francisco Gallardo amesema anatarajia kumuona mshambuliaji wa klabu ya Bayern MunichThomas Muller akijiunga na Magalaktiko wa Real Madrid.

Gallardo anaamini kuwa Muller, ambaye amesaini mkataba mpya na Bayern mara baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la Dunia kule nchini Brazil atakwenda kujiunga na Les Blancos akiwa kama mrithi wa mshambuliaji Karim Benzema anayetajwa kutaka kuondoka klabuni hapo.

"Thomas Müller ni mshambuliaji mkubwa na anaweza kucheza kwenye klabu yoyote ile Duniani na kutokana na vuguvugu la Benzema kutaka kuondoka kwenye kikosi hicho basi naamini Madrid watamgeukia mshambuliaji huyu ambaye ni mmoja kati ya washambuliaji wa kiwango cha juu kabisa Duniani."

Akiwa tayari amekwisha jitia kitanzi cha kuendele akubakia ndani ya kikosi cha Munich mpaka mwaka 2019 Muller ameshuhudiwa akiishia benchini kwenye michezo miwili iliyopita ya michuano ya UEFA Champions League  na hivyo kuongeza uwezekana wa mchezaji huyo kuanza kufikiria njia muafaka ya kujinusuru na benchi hilo lililoanza kumkabili.

Post a Comment

 
Top