0
Klopp: I won't resign
Kocha wa klabu ya Borussia Dortmund, Jurgen Klopp amekanusha vikali taarifa kuwa anampango wa kujiuzuru kuifundisha timu hiyo kufuatia kipigo ilichokipata siku ya jana cha jumla ya magoli 2-0 dhidi ya klabu ya Eintracht Frankfurt, kipigo ambacho kimeifanya klabu hiyo kushuka kwenye nafasi za chini kwenye msimamo wa ligi ya Bundesliga.

Magoli ya Alexander Meier na Haris Seferovic yaliipa klabu ya Frankfurt alama tatu muhimu na kuwasukuma BvB kwenye nafasi ya 18 kati ya timu 20 zinazoshiriki ligi kuu nchini Ujerumani ikiwa ni alama 22 nyuma ya vinara wa ligi hiyo klabu ya Bayern Munich.

Licha ya mwenendo huo mbaya bado meneja huyo ameendelea kusisitiza kuwa kamwe hajafikiria wala hafikirii kuiachia nafasi hiyo isipokuwa tu kama atatakiwa kufanya hivyo na wamiliki wa klabu hiyo na si kelele za mashabikiwala vyombo vya habari.

Mara baada ya mchezo huyo mashabiki wa klabu hiyo walionesha hisia zao za kusikitishwa na mwenendo wa timu yao kwani badhi walivamia uwanja na kuanza kuzungumza na wachezaji wakitaka kujua tatizo linalo isibu timu hiyo.

Baadhi ya wachezaji wa timu hiyo walionekana wakitokwa na machozi hali iliyoashiria kutoridhishwa na kutofahamu kwao na hali ya mambo inavyokwenda ndani ya klabu hiyo. 

Dortmund imekua moja kati ya vilabu gumzo kwa sasa ulimwenguni kutokana na uwezo mkubwa iliouonesha kwa miaka mitatu iliyopita kwenye ligi ya Bundesliga na hata ligi ya mabingwa barani Ulaya hivyo kuporomoka kwa ghafra kwa kiwango cha timu hiyo kunawaacha vinywa wazi wadadisi wegi wa masuala ya soka na hivyo kuanza kudhania kuwa ni wakati muafaka kwa meneja wa timu hiyo Jorgen klopp kuachia ngazi.

Post a Comment

 
Top