Klabu ya Manchester United imeripotiwa kufikia makubaliano ya kumrejesha nahodha wake wa zamani aliyetimuka klabuni hapo mapema mwaka huu Nemanja Vidic kutoka klabu ya Inter Milan ya nchini Italy mnamo mwezi wa January mwakani.
Vidic, mwenye umri wa miaka 33 kwa sasa aliondoka Manchester Unite mwishoni mwa msimu uliopita mara baada ya kumaliza mkataba wake ndani ya United na sasa anatarajiwa kurejea tena ndani ya viwanja vya United uhamisho ambao wadadisi wengi wa masuala ya soka wameonekana kuupinga kutokana na kiwango duni kilichooneshwa na mlinzi huyo kwa sasa akiwa na Inter.
Taarifa zinadai kuwa Meneja wa klabu ya Manchester United Luis van Gaal ameonekana kukubaliana na wazo hilo la kumrejesha mlinzi huyo mkongwe na taarifa zinadai kuwa mlinzi huyo atarejea klabuni hapo mapema mwezi ujao.
Post a Comment