Kocha wa klabu ya Arsenal Mfaransa Arsene Wenger amezungumzia uwezekano wa mshambuliaji wa zamani ya klabu hiyo anayekipiga kwenye klabu ya New York Red Bulls Thierry Henry kurejea tena ndani ya viwanja vya Emirates.
Ligendari huyo wa klabu ya Arsenal tayari amekwisha tangaza kutoongeza mkataba na klabu yake anayoitumikia kwa sasa ya New
York Red Bulls ya nchini Marekani, na taarifa zinadai kuwa mchezaji huyo yuko katika harakati za kustaafu kucheza soka kwa ujumla mzee Wenger anaamini kuwa mchezaji huyo atarejea kivingine kwenye viwanja hivyo vya Emirates.
‘Nadhani tunatakiwa tumpe muda wa kufanya tafakuri juu ya kile anachotaka kukifanya kwa sasa mara baada ya kuamua kustaafu kucheza soka, Ni shabiki mkubwa wa Arsenal, na alipokuwa hapa alikua na wakati mzuri sana ambao utaendelea kubakia kwenye kumbukumbu za masahabiki wengi wa klabu hii, Ninaamini kuwa siku moja atarejea hapa, kufanya kazi gani hilo ni jambo litakalojulikana muda ukifika cha maana ni sisi kwa ujumla wetu kumuacha afanye kile ambacho yeye binafsi amepanga kukifanya katika maisha yake mapya yajayo.
Post a Comment