0
Giggs in line to replace Mackay at Wigan
Siku za kuendelea kukinoa kikosi cha mashetani wekund wa Old Traford kwa meneja msaidizi wa timu ya Manchester United Ryan Giggs zinahesabika kutokana na ukweli kuwa klabu ya Wigan italazimika kumuajiri meneja mwingine ambaye atakuja kuziba pengo linalotarajiwa kuachwa wazi na meneja wa sasa wa klabu hiyo Malky Mackay ambaye analazimishwa na chama cha soka cha nchini Uingereza kuacha majukumu yake hayo.

Mackay anachunguzwa na FA kuhusiana na tuhuma zinazomkabili za kua alimtumia jumbe za picha za kibaguzi na matusi meneja mwenzake wakati akiwa meneja wa timu ya Cardiff City. Hivyo wakati uchunguzi huo ukindelea na hukumu itakapotolewa Mackay atatakiwa kujiweka kando na masuala ya kuongoza kandanda na hivyo Giggs anatajwa kama mrithi muafaka wa nafasi hiyo.

Mwenyekiti wa klabu ya Wigan Dave Whelan anamtazama Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Mnchester United kama ndiye mtu sahihi kushika nafasi itakayoachwa wazi na Mackay na inasemekana kuwa Giggs anatarajiwa kwenda na msaidizi wake Nicky Butt katika kuyatekeleza majukumu yake hayo mapya.

Post a Comment

 
Top