Wachezaji wawili raia wa Nigeria Vincent Enyeama na Ahmed Musa wamejitokeza kwenye orodha ya wachezaji watano wnaowania tuzo ya mchezaji bora wa bara la Afrika kwa mwaka 2014.
Wachezaji hao wametangazwa na shirikisho la soka barani Afrika CAF kutoka kwenye orodha ya awali ya wachezaji 25 waliotangazwa na shirikisho hilo mnamo mwezi wa 11 mwaka huu.
Wawili hao itawalazimu kutoana jasho na nahodha wa timu ya taifa ya Ghana Asamoah Gyan, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na mchezaji anayelishikiria taji hilo kwa sasa,Yaya Toure wa Ivory Coast.
Mara baada ya kutajwa kwa majina ya wachezaji hao wanaowania nafasi hiyo adimu kinachofuata ni shirikisho hilo la soka barani Afrika kutangaza majina matatu ya mwisho yatakayoingia kwenye fainali ambapo mshindi wake anatarajiwa kutangazwa kwenye mji wa Lagos nchini Nigeria mnamo tarehe 8 ya mwezi Januari mwakani.
Post a Comment