Mara baada ya kupata ushindi kiduchu kwenye dimba la the Hawthorns siku ya jumamosi, Meneja wa klabu ya Arsenal Mfaransa Arsene Wenger amekiri hadharani kuwa ili kupambana na kuirejeshea heshima ambayo inaonekana kuanza kutaka kupotea klabu ya Arsena ni lazima ahakikishe anamjumuisha kundini kiungo mmoja kwenye dirisha la usajili la mwezi Januari.
Kwenye mahojiano hayo aliyoyafanya kocha huyo wa klabu ya Arsenal bila ya kumtaja kiungo gani anayepanga kumjumuisha kikosini meneja huyo alikiri kuwa na tatizo la kiungo mkabaji kwenye kikosi chake na hivyo kutamka hadharani kuwa ni lazima amjumuishe kikosini kiungo mmoja mnamo mwezi wa Januari mwakani.
Viungo wakabaji kwenye dunia ya sasa wametoweka kabisa, Nadiriki kusema hivyo kwakuwa najaribu kuangalia uwezo wa watu wa kalba ya Mbarzil Emarson, Michael Essien, Roy Kean, Patrick Viera, Paul Ince na wengi wengineo wenye sifa zilizotukuka katika kufanya kazi ya kukaba kwenye vikosi vyao kwa nyakati hizo zilizotangulia.
Wako viungo wengi wanaojaribu kucheza kwa kiwango cha juu Duniani kwa sasa lakini tatizo linalokuja ni kupanda ghafla kwa bei za wachezaji hao jambo ambalo ninaliona kama ni tatizo kwa mzee Wenger; Ili kutatua tatizo linaloikabili Arsenal kwa sasa natamni kumuona mzee Wenger akiwajumuisha kikosini wachezaji wafuatao ili kuweka hali ya mambo sawa ndani ya timu hiyo.
1. Victor Wanyama
Victor Wanyama ni mmoja kati ya wachzaji waliokuwa wakihusishwa sana kujiunga na klabu ya Arsenal kabla ya dili hilo kuota mbawa na kumshuhudia kiungo huyo akitua kwenye kikosi cha Southampton mnamo mwezi Julai mwaka 2013 na kuonesha uhodari wa hali ya juu akiwatumikia watakatifu hao.
Kilichonifanya nijaribu kumpendekeza mchezaji huyu ni mara baada ya kupitia takwimu mbali mbaliza EPL ambazo zinamuonesha mchezaji huyu wa kiungo kuwa tayari amekwisha fanya tackling 34 huku akiweza kuzuia pasi 18 zisifike kwa adui ( Interceptions) ikiwa ni takwimu inayomkaribia kwa ukaribu kabisa kiungo wa klabu ya Chelsea Nemanja Matic mwenye tackles 36 na interceptions 18.
2. Fabian Delph
Fabian Delph anaweza asiwe chaguo la mashabiki wengi wa klbu ya Arsenal lakini pia hata kwa wale wasio mashabiki wa timu hiyo hususani kwenye majukumu ya kiungo mkabaji lakini nionavyo mimi thamani na umuhimu wake halisi watakuja kuuona pindi mchezaji huyo atakapokuwa mshika mtutu halisi ndani ya Emirates kama mpango utatimia.
Kiungo huyu wa zamani wa klabu ya Leeds United atakua amebakiza miezi sita tu kenye mkataba wake wa sasa utakapofika mwezi Januari na taarifa zinadai kuwa mchezaji huyo tayari amekwishaigomea Aston Villa kusainiana nayo mkataba mpya hivyo itawalazimu Aston Villa wamuuze mchezaji huyo ili waambulie chochote kuliko kukosa lolote.
3. James McCarthy
James McCarthy amesajiliwana klabu ya Everton akitokea timu iliyoshuka daraja ya Wigan Athletic. Mara tu baada ya kukabidhiwa majukumu ya kukinoa kikosi cha Toffees kutoka kwa meneja aliyetimukia klabu ya Manchester United David Moyes mwalimu wa sasa wa klabu ya Everton Roberto Martinez aliwaamuru mabosi zake wa Goodison Park kulipa ada ya paundi milioni 13 ili kumnasa kiungo huyo
Kitendo cha Everton kukubali kumnunua kiungo huyo kwa kiasi hicho cha pesa kilizua mjadala mkubwa sana miongoni mwa wachambuzi wa masuala ya soka wakidaia kuwa klabu ya Everton imelipa pesa nyingi sana kwaajili ya kumnyakua kiungo huyo.
James ameasuta wote waliokuwa wakimuona yeye kama galasa kwani ushirikiano wake na Gareth Barry kwenye sehenu ya kiungo cha klabu ya Everton uliifanya Everton ijikusajie jumla ya alama 72 msimu uliopita na kuingia kwenye rekodi ya moja kati ya vilabu vilivyowahi kumaliza ligi vikiwa na alama nyingi zaidi kwenye ligi ya EPL.
Post a Comment