Imearifiwa kuwa klabu ya Manchester United inajiandaa kutuma ofa ya kiasi cha paundi milioni 50 kwenda kwa klabu ya PSG ya nchini Ufaransa yenye lengo la kutaka kumng'oa mshambuliaji wa timu hiyo Edinson Cavani mara baada ya kuamua kutokumpa mkataba wa kudumu mshambuliaji Radamel Falcao.
Manchester United iko kwenye mipango ya kumsajili mshambuliaji anayekipiga kwa mkopo wa muda mrefu Radamel Falcao kutoka klabu ya Monaco kwa ada ya uhamisho ya Paundi milioni 50,Lakini maumivu ya muda mrefu ya mshambuliaji huyo raia wa Colombia yanamfanya meneja wa klabu ya Man Utd Louis van Gaal kumtoa kwenye mipango yake.
Taarifa kutoka nchini Ufaransa zinadai kuwa United inajiandaa kutuma ofa hiyo ili kumnasa huyo wa klabu ya PSG anayeonekana kutaka kukikimbia kivuli cha mshambuliaji mwenza wa timu hiyo Zlatani Ibrahimovich.
Post a Comment