Klabu ya Tottenham ya nchini Uingereza imepigwa faini ya kiasi cha paundi 11,870 na shirikisho la soka barani Ulaya, Uefa kutokana na kitendo cha mashabiki wake kuvamia uwanja kwenye mchezo wa michuano ya Europa League baina ya timu hiyo na klabu ya Partizan Belgrade mwezi uliopita.
Watu watatu wanaotajwa kuwa mashabiki wa klabu ya Tottenham walivamia uwanja na kuanza kupiga picha na baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo kwenye mchezo uliokuwa unachezwa kwenye dimba la White Hart Lane tukio ambalo lilisababisha mchezo huo kusimama kwa takribani dakika 10.
Mara baada ya tukio hilo klabu hiyo kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa Tweeter walilaani vikali tabia hiyo wakiita kuwa ni tabia isiyokubalika miongoni mwa wanafamilia wa mpira wa miguu na mara baada ya mchezo huo watua hao watatu wote walishikiriwa na jeshi la polisi kwaajili ya mahojiano zaidi.
Post a Comment