0
Suspended: Nigeria performed above expectations at the World Cup but are now banned from internationalsNchi 16 zinazotarajiwa kucheza fainali za michuano ya Mataifa ya Afrika hapo mwakani kule nchini Equatorial Guinea siku chache ujazo zitawajua wapinzani wao na makundi yao kutokana na droo itakayochezeshwa ya upangaji wa makundi hayo inayotarajiwa kufanyika Jumatano hii.

Makundi hayo yanayotarajiwa kupangwa huko nchini Equatorial Guinea kwenye mji wa Malabo, inatarajiwa kuoneshwa moja kwa moja na kituo cha luninga cha SuperSport cha nchini Afrika ya Kusini kupitia chanel zake za SS7HD, SS7, SS7N, na  Select . 

Timu zimegawanywa kwenye makundi manne ambayo kila kundi litaingia kwenye chungu chake kutegemeana na viwango vya FIFA vya mwezi uliopita. Timu moja kutoka kila chungu itaungana na timu mojamoja kutoka kila chungu na kutengeneza kundi moja. 

Kituo cha Luninga cha SuperSport kinatarajiwa kurusha moja kwa moja kutokea mjini malabo upangaji wa makundi hayo kuanzia mishale ya saa moja kamili usiku kwa saa za Afrika ya Mashariki.Mgawanyo wa timu kwenye vyungu upo kama ifuatavyo

Chungu namba 1.
 
Equatorial Guinea, Ghana , Zambia, Burkina Faso 

Chungu namba 2.
 
Ivory Coast, Mali, Tunisia, Algeria 

Chungu namba 3.
 
Cape Verde, South Africa, Gabon, DR Congo 

Chungu namba 4.
 
Cameroon, Senegal, Guinea, Congo

Post a Comment

 
Top