0
Arsenal's Diaby has apparently picked up a new 'serious' injury
Kiungo wa klabu ya Arsenal Abou Diaby ametajwa kuingia kwenye orodha ya majeruhi wa muda mrefu wa klabu hiyo mara baada ya hapo jana kupata maumivu mapya ya misuli ya paja aliyoyatwaa siku ya jana wakiwa mazoezini, maumivu yatakayomfanya kuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi mitatu.

Diaby ambaye bado hajarejea rasmi uwanjani kutoka kwenye maumivu yaliyomuweka nje ya uwanja kwa zaidi ya nusu msimu alikua akifanya mazoezi na timu yake hiyo katika hali ya kujiweka sawa kabla ya kurejea rasmi kazini na sasa kabla dhamira hiyo haijatimia imearifiwa kuwa mchezaji huyo amepata majeraha mengine ambayo yataifanya klabu yake ya Arsena isubirie mpaka mwezi January kuzipata huduma zake.

Msimu huu Diaby ameichezea klabu yake takribani michezo miwili tu mmoja ukiwa wa michuano ya Capita One Cup ambao klabu yake ilipoteza mbele ya Southampton na mwingine wa mwaka jana akitokea benchini ikiwa ni tangu alipopata majeraha ya kifundo cha mguu mnamo mwezi March 2013.

Post a Comment

 
Top